𝗝𝗲 𝘂𝗻𝗮𝗷𝘂𝗮 𝗠𝗮𝗮𝗻𝗮 𝘆𝗮 𝗣𝗜𝗗
Kwanza kabisa PID ni neno la kiingereza ambalo kirefu chake ni Pelvic Inflammatory Disease, yaani magonjwa ya maambukizi katika via vya uzazi vya mwanamke. Huwa ni tatizo ambalo mara nyingi huwachanganya watu kwani yaweza kuwa ni maambukizi ya zinaa, kama vile pangusa(Chlamydia) au Kisosono.
𝗡𝗨𝗞𝗨𝗨:
𝗞𝘂𝗺𝗯𝘂𝗸𝗮 𝗸𝘂𝘄𝗮, 𝘆𝗮𝗽𝗼 𝗺𝗮𝗮𝗺𝗯𝘂𝗸𝗶𝘇𝗶 𝗺𝗲𝗻𝗴𝗶𝗻𝗲 𝗮𝗺𝗯𝗮𝘆𝗼 𝘀𝗶𝗼 𝘆𝗮 𝘇𝗶𝗻𝗮𝗮 𝗹𝗮𝗸𝗶𝗻𝗶 𝘆𝗮𝗻𝗮𝘄𝗲𝘇𝗮 𝗸𝘂𝘀𝗮𝗯𝗮𝗯𝗶𝘀𝗵𝗮 𝗺𝗮𝘁𝗮𝘁𝗶𝘇𝗼 𝘆𝗮 𝗣𝗜𝗗.𝗝𝗲, 𝗨𝗻𝗮𝘄𝗲𝘇𝗮𝗷𝗲 𝗞𝘂𝗽𝗮𝘁𝗮 𝗣𝗜𝗗;
Na ieleweke kuwa, unaweza kupata matatizo ya PID endapo kama:
• Una magonjwa ya zinaa na hayajatibiwa
• Una mpenzi zaidi ya mmoja au michepuko
• Kuwa na mpenzi mwenye wapenzi wengi
• Uliwahi kuwa na PID kabla
• Unatumia marashi au vipodozi sehemu za uke
Je, Unawezaje Kupunguza Hatari Ya Maambukizi Ya PID?
Njia pekee ya kujihadhari na magonjwa ya zinaa ni kutokufanya mapenzi au ngono. Ikiwa kama unafanya ngono, basi unapaswa ufanye mambo yafuatayo ili kupunguza hatari ya maambukizi ya zinaa:
1. Kutumia kondom kila unapohitaji kufanya mapenzi
2. Kuwa na mpenzi ambaye tayari ameshapima na akaonekana hana maambukizi ya magonjwa ya zinaa
𝗝𝗲 𝘂𝗻𝗮𝘄𝗲𝘇𝗮𝗷𝗲 𝗸𝘂𝘁𝗮𝗺𝗯𝘂𝗮 𝗞𝘂𝘄𝗮 𝗨𝗻𝗮𝗺𝗮𝗮𝗺𝗯𝘂𝗸𝗶𝘇𝗶 𝘆𝗮 𝗣𝗜𝗗
Hivi leo katika hospitali mbalimbali huwa hakuna vipimo maalumu kwa ajili ya kupima na kutambua PID kwa haraka. Vipimo na uchunguzi mara nyingi huambatana na maelezo ya kihistoria ya afya ya mwili wako pamoja na matokeo mengine ya vipimo. Unaweza ukashindwa kugundua kuwa una PID kwa sababu dalili zako zinaweza zisionekane, au zikawa za kawaida tu kama vile za UTI au fangasi, na majibu ukapewa kuwa una UTI au fangasi. Hata hivyo, endapo kama utakuwa na dalili za PID, unaweza ukaona mambo kama haya:
• Maumivu maeneo ya tumbo la chini
• Kuhisi homa
• Kutokwa na uchafuukeni usio wa kawaida wenye harufu mbaya
• Kuhisi maumivu au kutokwa na damu wakati wa kujamiiana
• Kuhisi hali ya kuwaka moto wakati wa kukojoa
• Kutokwa na damu ya hedhi mara mbili ndani ya mwezi mmoja, nk
𝗝𝗲 𝘂𝗻𝗮𝗽𝗮𝘀𝘄𝗮 𝗸𝘂𝗳𝗮𝗻𝘆𝗮 𝗡𝗶𝗻𝗶?
• Pata vipimo haraka endapo kama utaona dalili zozote kama nilizozitaja
• Wahi kumuona daktari endapo kama utaona mwenzi wako ana maambuki
• Jitahidi kupima maambukizi ya pangusa(Chlamydia) kila mwaka
• Muone daktari mapema endapo kama utona unatokwa na uchafu mbaya ukeni
𝗝𝗲 𝗣.𝗜.𝗗 𝗜𝗻𝗮𝘄𝗲𝘇𝗮 𝗸𝘂𝘁𝗶𝗯𝗶𝗸𝗮 𝗻𝗮 𝗸𝘂𝗶𝘀𝗵𝗮 𝗸𝗮𝗯𝗶𝘀𝗮
Ndiyo, kama PID ikipimwa mapema, inaweza ikatibika kabisa. Hata hivyo, matibabu Tiba zetu zitaondoa Uharibifu wote ambao tayari umekwishajitokeza katika mfumo wako wa uzazi. Kadiri unavyozidi kuchelewa kupata matibabu, ndivyo tatizo linavyozidi kuongezeka. Unapokuwa ukitumia madawa ya vidonge, dalili za ugonjwa wa PID zinaweza zikatoweka kabla ya maambukizi hayajatibika tumboni mwako. Hata kama dalili zikiondoka, lakini unapaswa umalize dozi zako zote kabisa.
𝗡i 𝗺𝗮𝗱𝗵𝗮𝗿𝗮 𝗴𝗮𝗻𝗶 𝘆𝗮𝘁𝗮𝗺𝗽𝗮𝘁𝗮 𝗠𝗵𝘂𝘀𝗶𝗸𝗮 𝘂𝗸𝗶𝘄𝗮 𝗮𝘁𝗮𝗰𝗵𝗲𝗹𝗲𝘄𝗮 𝗸𝘂𝘁𝗶𝗯𝘂 𝘁𝗮𝘁𝗶𝘇𝗼 𝗵𝗶𝗹𝗶
Ikiwa kama utapata vipimo na kuanza kutiobiwa mapema, madhara ya PID yanaweza yakadhibitiwa. Baadhi ya madhara ya PID ni:
• Mimba kutunga nje ya kizazi
• Ugumba
• Maumivu makali ya nyonga
• Kupata michubuko kama vidonda nje na ndani ya mirija ya uzazi ambayo inaweza kusababisha mirija kuziba
𝗞𝘄𝗮𝗸𝘂𝗽𝗮𝘁𝗮 𝗧𝗶𝗯𝗮𝗹𝗶𝘀𝗵𝗲 𝘃𝗶𝗿𝘂𝘁𝘂𝗯𝗶𝘀𝗵𝗼 𝗮𝗺𝗯𝗮𝘃𝘆𝗼 𝗶𝘁𝗮𝗸𝘂𝗼𝗻𝗱𝗼𝗹𝗲𝗮 𝗸𝗮𝗯𝗶𝘀𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮𝗺𝗼𝘁𝗼 𝗵𝗶𝗶 𝗻𝗮 𝘇𝗶𝗻𝗴𝗶𝗻𝗲 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗠𝗮𝘀𝘄𝗮𝗹𝗮 𝘆𝗮 𝗨𝘇𝗮𝘇𝗶 𝗸𝗮𝗿𝗶𝗯𝘂 𝗸𝘂𝗽𝗮𝘁𝗮 𝗧𝗶𝗯𝗮 𝗕𝗼𝗿𝗮